Breaking News!!! Papa amechaguliwa Live fuatilia hapa
3:54 Papa mpya anaonekana ni Jorge Mario Bergoglio wa Argentina ndiye papa mpya
3:50 Gwaride la heshima limejipanga na kuimba wimbo wa taifa la Vatican anasubiriwa kiongozi wa makardinali aje amtangaze papa mpya
3:30 Band maalum inaanza kupita mbele ya kanisa kuu la St. Peter Basillica ni ishara papa mpya ataonekana hivi punde
3:26 Makelele na shangwe nje ya St. Peter Basillica
3:25 Makardinali waliokuwa wamejifungia tayari wamemchagua papa mpya ambaye atamriti papa Benedect wa 16 ambaye amestaafu.
Moshi mweupe umeonekana kwenye bomba la moshi ikiwa ni ishara kuwa makardinali wamekubaliana kumchagua mmoja wao kuwa papa.
Bado papa mpya hajatokea na kujulikana ni nani lakini tayari moshi mweupe umeshaonekana. Endelea kutufuatilia tutakuletea kila kinachoendelea muda mfupi ujao
Makardinali washindwa kumpata Papa siku ya kwanza
![]() |
| Moshi mweusi ukiashiria hakuna papa mpya aliyechaguliwa siku ya kwanza baada ya makardinali kujifungia katika hekalu maalum, huko Vatican City |
| Makardinali katika ibada katika kanisa la St. Peter Basillica kabla ya kujifungia kumchagua Papa hapo jana |
Siku ya kwanza ya uchaguzi wa papa mpya imeanza na hakuna dalili ya papa aliyechaguliwa baada ya moshi mweusi kuonekana angani kwenye bomba la moshi.
Zoezi la kumchagua papa atakayeongoza kanisa Katoliki duniani lilianza hapa jana Vatican City kwenye jumba maarufu la Sistine Chapel ambalo hutumika kwa ajili hiyo.
Makardinali wapatao 115 akiwepo Mudhama Policarp Kardinali Pengo wa Tanzania ni miongoni mwa walikusanyika kufanya zoezi hilo.
Yoyote kati ya makardinali hao anaweza kuwa papa mpya hivyo Kardinal Pengo naye ana nafasi ya kuwa papa mpya baada ya Papa Benedict xiv ambaye amestaafu.
Kwa sasa Papa Benedict amepewa jina jipya na ataitwa Papa Emaritus au Papa Emeritus wa Roma.
Kinachosubiriwa hapo kwa sasa ni moshi mweupe ambao ndio utakaonyesha papa mpya amepatikana na kama hajapatikana baada ya kupiga kura moshi mweusi utaonekana.
Makardinali hao watakaa katika jumba hilo hadi papa apatikane. Hawaruhusiwi kuwasiliana na mtu yoyote na watakuwa wakipiga kura mara nne kwa siku.
![]() |
| Mudhama Policap Kardinali Pengo (kulia) leo hii akiwa na Makardinali wenzake Vitican City |
![]() |
| Mudhama Policap Kardiali Pengo kushoto akiwa na mmoja wa makardinali hapo jana mjini Vatican |









Hakuna maoni:
Chapisha Maoni