Jumamosi, 16 Machi 2013

MATATANI KWA KUGUSHI SAHIHI NA KULAMBA MILIONI 2 ZA MAENDELEO



Watu wawali wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete kujibu tuhuma za kugushi sahihi na kuandika mhutasari wa kikao hewa na kuchukua zaidi ya shilingi milioni mbili katika akaunti ya mfuko wa maendeleo wa kata ya Bulongwa wilayani Makete
 Mwandishi wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Makete , Edwin Moshi anaripoti kuwa ,Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari ofisini kwake mwendesha mashitaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw. Frednandi Nsakuzi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni aliyekuwa diwani wa kata ya Bulongwa Estomin Mahenge na mwenzake Edwin Swallo ambaye alikuwa mtendaji wa kijiji cha Bulongwa ambapo mpaka anafanya tukio hilo alikuwa anakaimu ofisi ya mtendaji wa kata ya Bulongwa 
Watuhumiwa hao waligushi sahihi na kuandika mhutasari wa kikao hewa na kwenda katika benki ya Nmb tawi la Makete na kuchukua zaidi ya shilingi millioni mbili kwenye akaunti ya mfuko wa maendeleao ya kata ya Bulongwa wakidai kuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Usililo ambapo  mhutasari huo upo TAKUKURU

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani  hapo jana  kwa tuhuma hizo na walikana mashitaka yanayowakabili ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Machi 23 mwaka huu katika mahakama wilaya Makete na watuhumiwa hao wapo nje kwa dhamana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...